English to Swahili: Sports General field: Other Detailed field: Sports / Fitness / Recreation | |
Source text - English
MICHEZO-1 17/02/2014
Mabingwa wa ligi kuu ya soka humu nchini Gor Mahia, sasa watachuana na Esperence ya Tunisian, katika raundi ya kwanza kuwania ubingwa wa ligi ya mabingwa Barani Afrika.
Gor iliyoibandua US Bitam ya Gabon kupitia mikwaju ya penalti jana jijini Bitam, itamenyana na Esperance katika mkondo wa kwanza unaotarajiwa kuandaliwa tarehe moja au mbili mwezi ujao; huku mchuano wa marudiano ukiandaliwa baada ya juma moja. Ushindi kwa Gor Mahia utaifuzisha kwa raundi ya pili kuchuana na aidha, Enyimba ya Naijeria au AS Real Bamako ya Mali. Mshindi katika raundi ya pili atajikatia tikiti ya kushiriki katika awamu ya makundi. Gor Mahia inatarajiwa kurejea jijini Nairobi leo jioni; na Alhamisi itaanza harakati za kutetea taji yao ya ligi kuu dhidi ya City Stars uwanjani City. AFC Leopards ambayo pia ilifuzu kwa raundi ya pili ya kombe la mashirikisho barani Afrika kwa kuibandua FC Defense ya Ethiopia kwa jumla ya mabao 4-1, sasa itakabiliana a Super Sports United ya Afrika Kusini, tarehe mbili mwezi ujao katika mkondo kwanza utakaochezwa nchini Afrika Kusini. AFC Leopards itaanza harakati zake za kuwania ligi kuu dhidi ya KCB Jumatano katika uwanja wa taifa wa Nyayo.
| Translation - Swahili SPORTS-1 LLLLLLLLLLLLLLLLL 17/02/2014
Kenyan Premier League Champions Gor Mahia will now face Tunisian side Esperance in the Africa Champions League First round.
Gor who eliminated US Bitam of Gabon via post match penalties yesterday in Bitam will take on Esperance in the first leg on the weekend of 1st and 2nd of March with the return leg scheduled for a week later. A win for Gor Mahia in the two-legged tie will push them to the second round where they will meet either Enyimba of Nigera or AS Real Bamako of Mali. The winner in the second round qualifies for the group stage. Gor Mahia are expected in the country this evening, On Thursday, they will kick of their Kenyan Premier League title defense against City Stars at City Stadium. AFC Leopards who qualified for the second round of the confederations Cup after ousting FC Defense of Ethiopia 4-1 on aggregate will now play Super Sports United of South Africa on 2nd March in their first leg away in South Africa. AFC will shift their attention back to the local league where they are expected to face KCB on Wednesday at the Nyayo national stadium in their first domestic league match of 2014 campaign.
|