Nyakati za ukuaji wa ghafla wa biashara zimerejea katika Bonde la Silicon. Viwanja vya ofisi kando ya Barabara kuu ya 101 vimepambwa kwa mara nyingine tena na alama za mianzo yenye matumaini. Kodi za nyumba zinapanda kwa haraka, kama yalivyo mahitaji ya nyumba nzuri za likizo katika miji ya matembezi ya kutalii kama Ziwa Tahoe, ishara ya utajiri ukikusanywa. Eneo la Bay lilikuwa mahali pa kuzaliwa kwa tasnia ya vifaa vipitisha-nusu (semiconductor) na kampuni za kompyuta na mtandao wa intaneti ambazo zimekua kwa sababu yake. Wataalamu wake walitoa maajabu mengi ambayo yanafanya ulimwengu uwe wa kisasa zaidi na kustaajabisha, kuanzia simu za skrini za kugusa hadi utafutaji wa papo hapo wa maktaba kubwa na nguvu ya kuendesha droni umbali wa maelfu ya maili. Ufufukaji katika shughuli zake za biashara tangu 2010 unaonyesha maendeleo yanaongezeka kwa kasi.
Hivyo inaweza kuwa mshangao kwamba wengine katika Bonde la Silicon wanafikiria mahali hapo pamedumaa, na kwamba kiwango cha uvumbuzi kimedorora kwa miongo kadhaa. Peter Thiel, mwanzilishi wa PayPal, na mwekezaji wa kwanza wa Facebook, anasema kwamba uvumbuzi huko Amerika upo "mahali fulani hivi kati ya hali ngumu na wafu". Wahandisi katika kila aina ya maeneo hushiriki hisia kama hizo za kukata tamaa. Na kikundi kidogo lakini kinachokua cha wachumi kinachochukulia athari za kiuchumi za uvumbuzi wa leo kinaweza kisifue dafu/kisifikie kwa wale wa zamani.
Kwa ngazi zote na kila mahali, vumbuzi zinazochochewa kwa nguvu ya gharama nafuu ya utekelezaji hatua zinafanikiwa. Kompyuta zinaanza kuelewa lugha asilia. Watu wanadhibiti michezo ya video kwa utembezaji wa mwili pekee - teknolojia ambayo inaweza kupata matumizi katika sehemu nyingi za biashara. Uchapishaji wa pande tatu unaweza kufyatua mpangilio mgumu zaidi wa vitu, na hivi karibuni unaweza kuhamia kwenye tishu za kibinadamu na vitu vingine vyenye asili ya viumbe.
Mtu mwenye shaka kwa uvumbuzi anaweza kudharau hili eti ni “ahadi za kesho zisizotimia”. Lakini wazo kwamba ukuaji unaoongozwa na teknolojia lazima uendelee bila kupungua au upungue polepole, badala ya kupanda na kushuka, haliendani na historia. Chad Syverson wa Chuo Kikuu cha Chicago anasema kwamba ukuaji wa uzalishaji kipindi cha matumizi ya umeme ulikuwa wa kiasi kikubwa. Ukuaji ulikuwa polepole wakati wa uvumbuzi muhimu wa umeme mwishoni mwa karne ya 19 na mapema karne ya 20; kisha ukaongezeka ghafla.